Nafasi Mpya 17 za Kazi Kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Agusti 2024
Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019. Ni taasisi yenye jukumu la kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao pamoja na kuhimiza utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa taasisi za umma.
Kuanzishwa kwa Mamlaka hii mwaka 2019 kunaendeleza afua za Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na kuchukua sehemu ya mipango yake kwa sababu majukumu ya taasisi hizi yanafanana ingawa yanatofautiana katika mamlaka ya utendaji.

Mamlaka ya Serikali Mtandao ni taasisi iliyoirithi Wakala ya Serikali Mtandao iliyoundwa Aprili 2012 kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 Sura ya 245 ya mwaka 1997 yenye jukumu na Mamlaka ya Kuratibu, Kusimamia na Kukuza Jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.
Kabla ya kuanzishwa Wakala ya Serikali Mtandao, matumizi ya TEHAMA Serikalini yalikuwa yanaratibiwa na kusimamiwa na Idara ya Usimamizi wa Mifumo (DMIS) iliyopo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambayo kwa sasa ni Idara ya Huduma za TEHAMA Serikalini (DICTS).
Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019 imeainisha majukumu na mamlaka yanayoiongoza Mamlaka ya Serikali Mtandao katika utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini Tanzania.
Dira
Kutambuliwa kuwa taasisi inayoongoza kwa ubunifu katika kuwezesha matumizi ya TEHAMA kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma kwa umma.
Dhamira
Kujenga mazingira wezeshi ya kisheria kwa ajili ya uratibu, usimamiaji na uendelezaji wa matumizi ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa umma.
Nafasi Mpya 17 za Kazi Kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Agusti 2024
Ili kuweza kutuma maombi yako tafadhari bonyeza linki kwenye kila posti hapo chini;
- ICT OFFICER GRADE II (PROJECT MANAGEMENT) – 2 POST
- ICT OFFICER II (APPLICATION PROGRAMMERS) – 6 POST
- ICT OFFICER II (SYSTEMS ADMINISTRATOR) – 2 POST
- ICT OFFICER GRADE II (BUSINESS ANALYST),. – 1 POST
- ICT OFFICER GRADE II (SECURITY MANAGEMENT) – 1 POST
- ICT OFFICER GRADE II (STANDARDS AND COMPLIANCE) – 2 POST
- ICT OFFICER GRADE II (HELPDESK) – 2 POST
- ICT OFFICER GRADE II (DATA ANALYST) – 1 POST