Nafasi za kazi Afisa Ununuzi Daraja La II Kutoka MDAs na LGAs Nafasi 350 August 2024
Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
AFISA UNUNUZI DARAJA LA II (PROCUREMENT OFFICER II) – NAFASI 350
MAJUKUMU YA KAZI
i. Kushiriki katika kuandaa nyaraka za zabuni;
ii. Kusambazi hati/nyaraka za zabuni;
iii. Kuwasiliana na idara mbalimbali kuhusu mahitaji ya ununuzi;
iv. Kukusanya na kutunza taarifa ya bei za soko (Market Intelligence) kwa baadhi ya bidhaa;
v. Kuhakiki hati zote za madai kabla ya malipo; na
vi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Ununuzi au Ugavi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au wenye “Professional level Ill” inayotolewa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Professionals and Technicians Board (PSPTB)); au sifa nyingine inayotambuliwa na PSPTB na awe aliyesajiliwana PSPTB kama “Graduate Procurement and Supplies Professional”.
NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/.= (Anuani hii pia inapatikanaMkwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.