MABADILIKO ya Eneo la Usaili wa Vitendo Kada ya Afisa Mambo ya Nje Daraja la II
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, anawajulisha waombaji kazi wa kada ya AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II (FOREIGN SERVICE OFFICERS) kuwa kuna mabadiliko ya sehemu ya kufanyia usaili wa vitendo.
Usaili utafanyika OFISI ZA SEKRETARIETI YA AJIRA(PSRS)-DODOMA, MTAA WA MAHAKAMA, ENEO LA TAMBUKARELI badala ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP)- DODOMA Aidha, Muda na tarehe unabaki kama ilivyokuwa kwenye tangazo la awali la kuitwa kwenye usaili.