TAARIFA Kwa Walioitwa kwenye Usaili wa Tarehe 28-29 Julai, 2025
Wasailiwa wote mlioitwa kwenye usaili utakaofanyika kwa njia ya mtandao (ONLINE) tarehe 28 – 29 Julai 2025, mnatakiwa kuhuisha (update) taarifa katika akaunti zenu za ajira portal, kwa kuainisha mahali ulipo kwa sasa ili
upangiwe kituo cha usaili karibu na eneo lako.
Ili kuhuisha taarifa zako – nenda kwenye eneo la PERSONAL DETAILS, kisha rekebisha eneo la CURRENT RESIDENT REGION kwa kuandika Mkoa na Wilaya uliyopo kwa sasa. Na kwa wale ambao hawajaitwa kwenye usaili kwa sababu mbalimbali, endapo watataka kukata rufaa – wanaweza kuwasiliana na kituo cha Huduma kwa wateja namba 0262160350 au kwa barua pepe [email protected] / [email protected] mwisho wa zoezi hili ni Julai 21,
2025.
Tembelea Tovuti ya www.ajira.go.tz kwa maelezo zaidi.