Jinsi Ya Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv kupita Mitandao Ya Simu kama Airtel Airtel Money, Vodacom M-pesa, Halopesa na Tigo pesa 2024
Habari ya wakati huu ewe mtumiaji wa king’amuzi cha Azam Tv, karibu katika makala hii itakayoenda kukupa mwongo wa jinsi ya kulipia vifurushi vya king’amuzi cha Azam Tv kwa kutumia mitandao mbali mbali ya simu kama vile vodacom, Airtel, Halotel na tigo
Kisimbuzi cha Azam Tv kimeokua kisimbuzi pendwa zaidi nchini Tanzania kutokana na maudhui yanayotolewa na channel zilipo kwenye kisimbuzi hicho
Maudhui Ya Channel Za Azam Tv
Kuna maudhui ya aina mbali mbali yanayopatikana kwenye visimbuzi vya king’amuzi cha Azam Tv, Mfano wa maudhui hayo ni pamoja na;
- Maudhui ya Michezo
- Maudhui ya Elimu
- Maudhui ya Kidini
- Maudhui ya Burudani
Aina ya Visimbuzi Vya Kingamuzi Cha Azam Tv
Kuna aina kuu mbili ya visimbuzi katika king’amuzi Aazm Tv, Aina hizo ni’
- Kisimbuzi Cha Dishi
- Kisimbuzi Cha Antena
Jinsi Ya Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv kupita Mitandao Ya Simu
Kama tuliyosema hapo awali kua katika makala hii tutaenda kuangalia jinsi ya kulipia vifurushi vya king’amuzi cha Azam Tv kwa kupitia mitandao ya simu.
Njia Za Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv
Kuna njia mbali mbali za kuweza kulipia kifurushi chako cha Azam Tv , Miongoni mwa njia hizo ni pamoja na
- Kulipia kwa kutumia wakala
- Kulipia kwa kutumia mitandao ya Simu
- Kulipia kwa njia ya Benki
- Kulipia kwa kupiga simu Azam huduma kwa wateja
- Kulipia kwa kutembelea ofisi ya Azam Tv
Hapa tutaenda kuangalia njia ya kulipia kingamuzi cha Azam Tv kwa kutumia mitandao ya simu
Jinsi Ya Kulipia King’amuzi Cha Azam Tv Kwa Vodacom
Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa vodacom basi hapa chini tumekuwekea njia rahisi/hatua za kufanya ili kuweza kulipia kifurushi cha king’amuzi chako cha Azam Tv. Cha kufanya fuata hatua hizi kwa umakini zaidi
- Piga *150*00# kwenye simu yako
- Chagua “Lipa kwa M-Pesa”
- Chagua Namba 4 – Malipo Ya Kampuni
- Chagua Namba 3 – Chagua Kwenye Orodha
- Chagua Namba 1 – King’amuzi
- Chagua Namba 5 – Azam TV
- Ingiza Namba Ya Kumbukumbu
- Weka Kiasi cha Malipo
- Ingiza Namba Yako Ya Siri ya M-Pesa
- Bonyeza 1 ili kuthibitisha
Jinsi Ya Kulipia Azam Tv Kwa Airtel Money
- Piga *150*60#
- Chagua Lipa Bili
- Chagua chagua biashara
- Chagua Vin’gamuzi vya TV
- Chagua Azam Pay TV
- Weka kiasi
- Weka Nambari ya Marejeleo (Nambari ya Akaunti ya Azam TV)
- Weka Pini
- Bonyeza 1 ili kuthibitisha
Jinsi Ya Kulipia Azam Tv Kwa Tigopesa
- Piga *150*01#
- Chagua Lipa Bili
- Chagua Pata nambari ya biashara
- Chagua 5 kin’gamuzi ( Usajili wa TV)
- Chagua Azam Pay Tv
- Chagua Ingiza Kumbukumbu namba
- Weka namba yako ya Akaunti ya Azam TV
- Weka kiasi
- Weka pini
- Bonyeza 1 ili kuthibitisha, 2 ili kukataa
Kwa maelezo zaidi tafadhali angalia video hapa chini
Mapendekezo Ya Mhariri
1. Jinsi ya Kujiunga na Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI
2. Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu
3. Orodha Ya Shule Za Sekondari Mkoa wa Morogoro