Kama tujuavyo vijana waliowengi pindi wanapohitimu daraja flani la elimu huwa ni matamanio yao kupata ajira serikalini au katika taasisi yoyote ile ya kiserikali, hii ni kutokana na mazingira mazuri ya mahara pa utendaji kazi yanavyoandaliwa na unono wa mishahara kwa wafanyakazi wa serikali pia usala katika mazingira ya kazi.
Kiwango cha wahitimu na watafuta ajira kwenye taasisi za kiserikali ni kikubwa kuliko mahitaji au ajira zinazotangazwa hivyo kusababisha umati mkubwa wa wahitaji ajira kila mwaka.Hivyo basi ifahamike kua kwa muhitimu yeyote yule iwe wa kidato cha nne, sita au elimu ya juu kama matarajio yako ni kupata ajira serikalini au katika taasisi yoyote ile ya kiserikali basi mfumo wa ajira TAMISEMI (TAMISEMI Job Application System) ndio chaguo lako la kwanza kwa maana mfumo huu unakufanya mtumiaji kutuma maombi ya kazi kwa urahisi zaidi pia nafasi za kazi kutoka taasisi zote za kiserikali huchapishwa ndani ya mfumo huu.
Mfumo huu wa Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa kwa kifupi TAMISEMI ulianzishwa kwa lengo la kuharakisha mchakato mzima wa waombaji wa ajira serikalini katika ngazi ya serikali za mitaa.
JIUNGE NA WHATSAPP CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA WHATSAPP GROUP LETU HAPA,
Jinsi ya Kujiunga na Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI
Kama tujuavyo kua hapo awali utumaji wa maombi ya ajira hasa zilizo chini ya halmashauri ilikua nichangamoto kubwa sana hasa kwa upande wa gharama za utumaji maombi pia hata matumizi ya muda mrefu katika kutuma maombi, hivyo basi serikali kwa kuliona hilo ikaleta mfumo wezeshi wa kielekitroniki ambao kwa ujumla haumpi tena mwombaji ajira utumiaji wa peni na karatasi au kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa lengo la kupeleka maombi ya ajira bali uandaaji wa cv, usajili na hata utafutaji na utumaji wa maombi ya ajira vyote kwa sasa vinafanyika kwa njia ya kimtandao.
Katika mfumo wa ajira TAMISEMI , serikali kupitia halmashauri zake na taasisi za kiserikali hutuma nafasi za ajira zote katika mfumo huo, hivyo mwombaji wa ajira kupitia mfumo wa ajira hupata fursa ya kutazama ajira mbali mbali zilizotangazwa na taasisi tofauti tofauti kitu ambacho humpa uwanda mpana mtafuta ajira kulingana na kile alicho somea.
Licha ya mfumo huu kuwa na uwezo wa kuchapisha nafasi za kazi kutoka taasisi tofauti tofauti za kiserikali lakini pia hubeba taarifa zote za kimsingi juu ya bnafasi hiyo ya kazi iliyotangazwa kama vile sifa za mwobaji,pia hunyesha siku ilipochapiswa na mwisho wa kutuma maombi.
Kama tulivyosema hapo awali katika Makala hii tutaenda kujadili kuhusu unavyoweza kutengeneza akaunti, jinsi ya kutafuta nafasi mbali mbali za kazi katika mfumo wa jira TAMISEMI, njinsi ya kutengeneza cv na jinsi ya kuhakikisha unatuma maombi yako ya kazi kwa usahihi.
Vitu vya msingi kabla ya kujiunga na mfumo wa Ajira TAMISEMI
Unapofikilia kujiunga na kuanza kutumia mfumo wa jira wa TAMISEMI lazima uwe umejiandaa vya kutosha ili kuhakikisha unapoingia kwenye mfumo na kuanza kujisajili hadi kufikia kutuma maombi yako ya kazi hakuna kitakacho kukwamisha, hivyo hakikisha unavitu vifuatavyo ili kuanza matumizi ya mfumo wa Ajira wa TAMISEMI;
1.Nyaraka zinazohitajika,
Kunanyaraka muhimu itakuhitaji uwenazo pindi unapoanza kujisajiri katika mfumo wa ajira TAMISEMI, hivyo hakikisha nyaraka hizo unazo kwa wakati huo.
Mfano ni; – Vyeti vyako vya kielimu (kidato cha nne, sita na elimu ya juu)
2. cheti cha kuzaliwa
3. Kitambulisho cha Taifa (namba ya NIDA) au leseni ya udereva kama itahitajika
Kumb; Kwa vyeti vyako vya shule hakikisha vimepigwa muhuri wa mwanasheria kabla haujavitumia katika mfumo wa ajira.
- Nyaraka zote hakikisha umeziweka kwenyemfumo wan akala za kidijitali katika fomati ya PDF, kwakufanya hivyo itakurahisishia kuvipakia vyeti vyako kwenye mfumo kiurahisi zaidi kwani kinachohitajika kuwekwa katika mfumo wa jira ni nakara tepe.
- Kitu cha mwisho na ndio cha muhimu zaidi ni Internet
Hakikisha unakifaa ambacho kinaruhusu matumizi ya intaneti lakini pia uwe katika mazingira ambayo upatikanaji wa mtandao wa intaneti ni rahisi na sio wa kusua sua hii itakusaidia kufanya zoezi lako kwa wakati lakini pia itasaidi mfumo wa ajira kufunguka kwa wepesi na haraka zaidi.
Jinsi ya Kutengeneza Akaunti Kwenye Mfumo wa Ajira wa TAMISEMI
Bada ya kuhakikisha tayari unavitu vyote vya msingi hasa kifaa kinachoweza kukuwezesha kuingia mtandaoni iwe simu au kompyuta sasa hatua inayofuta ni kufungua akaunti na kujisajiri katika mfumo wa Ajira TAMISEMI(AJIAR PORTAL)

Kujisajili katika mfumo wa ajira wa TAMISEMI ni rahisi sana kwasababu huitaji taarifa chache sana ila za kimsingi, sasa ili kujisajili tumekuletea hatua za kufuata hapa chini;
1-Kwanza kabisa kupitia kifaa chako cha intaneti ingia kwenye mfumo wa google nafungua wavuti ya Ajira TAMISEMI kupitia linki hii hapa portal.ajira.go.tz
2- Baada ya kufungua hiyo wavuti mfumo wa ajira utafunguka kisha bonyeza paripo andikwa “JISAJILI” au “UNDA AKAUNTI”
3- Kisha jaza taarifa zako za msingi kwa usahihi hakikisha unacho jaza hapa hakitofautiani hata kidogo na taarifa zako, kama jina lako kamili,anuani ya makazi,tarehe yako ya kuzaliwa, namba ya simu pamoja na barua pepe yako.
4-Weka neno siri (password), hakikisha unaweka neno siri ambalo si rahisi zaidi kwa mtu mwingine kulifikilia kiurahisi na kuweza kulitumia katika akaunti yako, angalizo usipenede kutumia mwaka wako wa kuzaliwa kama neno siri lako kwani ni rahisi sana kufikilika.
–Thibitisha akaunti, hii ni hatua ya mwisho katika kuunda akaunti yako kisha utapokea barua pepe yenye kiungo cha kuthibitisha akaunti yako. Bofya kiungo hicho ili kukamilisha usajili.
Jinsi Ya Kujenga Wasifu Wako
Hii ni hatua ya muhimu sana kwa mtu yoyote yule atafutae ajira iwe ndani ya mfumo wa ajira hata nje ya mfumo wa ajira kwakua wasifu wako ndio unaokutambulisha moja kwa moja kwa mwajiri wako juu ya uwezo wako katika kazi unayo iomba, hivyo basi kupitia mfumo wa ajira hakikisha umejaza kwa ukamilifu wa hali ya juu wasifu wako pasipo kua na dosali ya aina yoyote kwa mapungufu yoyote kwenye wasifu wako yanaweza kukufanya ukakosa ajira.
-Kujaza wasifi wako unachotakiwa kufanya ni kuingia katika akaunti yako uliojisajili kupitia barua pepe yako au namba za NIDA au kitambulisho cha taifa na neno siri uliloliunda.
-Kisha ukiwa ndani ya mfumo hakikisha unaongeza baadhi ya taarifa zako za kimsingi kama vile taarifa za kielimu kuanzia shule ya msingi hadi elimu ulio hitimu kwa kuambatanisha na nakala za kuhitimu kila daraja la elimu, shule na mwaka wa kuhitimu kwa kila ngazi ya elimu uliofikia.
Pia hakikisha umeweka ujuzi na uzoefu wa kazi unao iomba, toa maelezo kwa kiasi gani unauzoefu na hiyo kazi kama ulisha wahi kuifanya hapo awali pia ujuzi wa ziada katika kazi hiyo kama matumizi ya kompyuta, lugha za kigeni na hata kama unafani yoyote ile.
Hakikisha pia unaweka picha yako ya pasipoti, picha utakayoiweka hakikisha inakuonyesha vizuri kwani pia hutumika katika wasifu wako, mwonekano wa picha yako pia unaweza kuchangia nafasi yako ya kupata ajira au kukosa kabisa kwahiyo hakikisha unachagua picha yenye ubora zaidi.
Jinsi ya Kutafuta Nafasi za Ajira Katika Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI
Mfumo wa ajira wa TAMISEMI ni mfumno ambao kila siku huchapisha nafasi mpya za kazi kutoka katika taasisi tofauti tofauti ili kutafuta kazi uitakayo tumia mfumo wa kategoria ambao utakupa urahisi zaidi kulingana na sifa zako za kitaaluma
Tumia kategoria; Katika uwanja wa mbele(homepage) ya mfumo wa ajira, machapisho yote ya ajira huwekwa kwa kuzingatia aina ya kategoria, ili uweze kupata ajira ya taaluma yako nenda katika kategoria ya ufanisi wako,
Mfano mtu anayetafuta ajira ya uwalimu ataenda katika kategoria ya “EDUCATION AND TRAING”

Baada ya kupata kazi unayoitaka hakikisha unasoma amelezo ya ajira hiyo kwa makini kabla hujatuma maombi yako hii itasaidi kutokukupotezea mda kwa kutuma maombi katika nafasi ya kazi usiyokua na sifa na vigezo nayo.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Mara baada ya kujithibitishia juu ya nafasi ya kazi uliyoitafuta kua inalingana kabisa na vigezo ulivyonavyo sasa unaweza kutuma maombi yako, hapa chini tumekuletea hatua za kufuata ili kuhakikisha unatuma maombi yako kwa usahihi kabisa;

1.Kwenye ukurasa wa maelezo ya ajira husika bonyeza kitufe kilichoandiwa tuma maombi (Apply)
2.Hakikisha unaambatanisha na barua ya maombi ya kazi, kumbuka barua ya maombi ya kazi iandike kwa mkono na kisha ibadili kwenda nakala tepe na upakie kwenye mfumo.
3.Thibitisha maombi yako, hakikisha umepitia taarifa zako zote kuona kama ziko sahihi na zimekamilika kulingana na mahitaji ya kimsingi ya nafasi hiyo ya kazi. Kama yako sahihi kisha bonyeza neno TUMA ili kutuma maombi yako
Mapendekezo ya Mhariri;
1. Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa Simu
2. Jinsi ya Kuweka Pesa Kwenye Kadi ya Mwendokasi
3. Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari Yako Kwa Urahisi Zaidi
4. Fahama Jinsi Ya Kutumia Kadi Ya Mwendokasi
Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa unamaswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.
Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku
BONYEZA HAPA