NAFASI 11 za Kazi Makambako Town Council
Halmashauri ya Mji Makambako imepokea kibali cha Ajira mpya chenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kwa nafasi ya Dereva Daraja la II, Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi kama ilivyoorodheshwa katika tangazo hili.
NAFASI 11 za Kazi Makambako Town Council
Nafasi zilizopo
- DEREVA DARAJA LA II – NAFASI- 6
- MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 1
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
MASHARTI YA JUMLA
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania, wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa,
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye Anuani, Namba za Simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminika,
iv. Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya Kidato cha Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye Ajira Portal,
v. Testimonials “Provision Results”, “Statement of Results” Hati ya Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita HAVIKUBALIKI,
vi. Waombaji kazi wa kada ya Dereva II wenye leseni Daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika
vii. Waombaji wote waweke picha mbili “Passport Size” ya hivi karibuni katika ukurasa wa Ajira Portal,
viii. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika yaani TCU, NECTA na NACTE,
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi,
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka wenye Kumb. Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010,
xi. Uwasilishwaji taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria,
xii. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 01 Julai, 2025