TAMISEMI: FORM FIVE SELECTION 2025/2026

_________________________________________________

MATANGAZO YA AJIRA  KILA SIKU BOFYA HAPA

_________________________________________________

NOTES ZA KIDATO CHA 1 HADI 6 BOFYA HAPA

_________________________________________________

MAGROUP MAPYA YA WHATSAAP BOFYA HAPA

_________________________________________________
MATANGO YA AJIRA BOFYA HAPA
JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA

NAFASI za Kazi Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II Muheza District Council

Filed in Nafasi Za Kazi Tanzania 2025 by on June 19, 2025 0 Comments

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025

NAFASI za Kazi Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja II Muheza District Council

MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II – NAFASI 05

KAZI NA MAJUKUMU

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na Siri
ii. Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
iii. Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine.
iv.Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
vi.Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
vii.Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi na
ix.Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe na Elimu ya kidato cha Nne au Sita mwenye Stashahada ya Uhazili au cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za Komputa za Ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya serikali yaani TGS C.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 01 Julai, 2025,

➢ MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, Anuani ya barua hiyo ielekeze kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Muheza,
S.L.P. 20,
MUHEZA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

 

Kwa Matangazo ya AJIRA Mpya kila siku BONYEZA HAPA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!