NAFASI 8 za Kazi Ikungi District Council
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amepokea kibali cha Ajira mpya chenye Kumb Na. FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025 kutoka kwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Hivyo anatangazia Watanzania wote wenye Sifa kutuma maombi kwa nafasi zilizopo.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
➢ Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 na umri usiopungua miaka 18,
➢ Waombaji waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa
➢ Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani, namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminika,
➢ Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya Taaluma na vyeti vya kidato cha Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye Mfumo wa Ajira Portal
➢ Testimonials “Provision Results”,” Statement of Results” Hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Sita HAVITAKUBALIKA,
➢ Waombaji wote waweke picha mbili “Passport Size” ya hivi karibuni katika ukurasa wa Ajira Portal
➢ Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika yaani TCU, NECTA na NACTE
➢ Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
➢ Waombaji kazi wa kada ya Dereva Daraja la II wenye leseni daraja E au C wanapaswa KUAMBATISHA vyeti vya mafunzo ya Udereva vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja husika.
➢ Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka kwenye Kumb. Na.CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 29 Novemba, 2010.
➢ Uwasilishwaji taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria,
➢ Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 01 Julai, 2025