Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga
Hatimaye timu ya Ts Galaxy ya ligi Kuu ya afrika ya kusini imekubali juu ya mchezo wao dhidi ya timu Young Africans uweze kuonyeshwa kwenye Tv kama ilivyoombwa na klabu ya young Africans.
Hii imekuja wakati timu hiyo ilipokataa mchezo huo usiweze kurushwa kwenye runinga. Baada ya timu ya young Africans kuomba mchezo huo kuweza kurushwa live kupitia TV ndipo timu ya Ts Galaxy ikakubali mchezo huo uonyeshwe live.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa siku ya jumanne ya tarehe 24 Julai 2024 na utarushwa live kupitia Azam Sport 1 HD saa 10:00.
Kwa klabu ya young Africans huu utakua mchezo wake wa pili wa pre season. Mchezo wake wa kwanza alicheza dhidi ya Augsburg ya uberigiji na kupoteza kwa kufugwa goli 2 kwa Moja 1.