MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wila ya Kalambo

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wila ya Kalambo

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi ya Msaidizi wa Kumbukumbu kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 27.06.2025 hadi tarehe 28.06.2025 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wila ya Kalambo

1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.

2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)

3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;

4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.

5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.

6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.

7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.

8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.

9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.

11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.

12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

13. Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa hali ya hewa ya Wilaya ya Kalambo ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri ya Wila ya Kalambo

Ili kuweza kusoma majina yote ya walioweza kutwa kwenye usaili Halmashauri ya wilaya ya Kalambo June 2025 tafadhari embu bonyeza kwenye linki hapo chini;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!