Kwa AJIRA Mpya Kila Siku (BOFYA HAPA)

_____________________________________

MAMBO ya Muhimu Fomu ya Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama June 2025

MAMBO ya Muhimu Fomu ya Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama June 2025

Mambo ya kujaza kwenye fomu ya maombi ya Ajira tume ya utumishi wa Mahakama, Judicial Service Commission – Application Form 2025

MAMBO ya Muhimu Fomu ya Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama June 2025

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo huru kilichoundwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kusimamia masuala ya ajira na maendeleo ya watumishi wa Mahakama. Tume hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa ajira, mafunzo, kupandishwa vyeo, pamoja na nidhamu ya watumishi wa Mahakama vinafanyika kwa haki, uwazi, na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora. Kwa kufanya hivyo, Tume husaidia katika kuimarisha ufanisi wa huduma za kimahakama na kuleta imani kwa wananchi kuhusu mfumo wa utoaji haki nchini.

Majukumu ya Tume hayaishii tu kwenye kusimamia ajira bali pia huchukua hatua za kiutawala katika kushughulikia malalamiko dhidi ya watumishi wa Mahakama, kuhakikisha uwajibikaji na maadili ya kazi yanafuatwa. Pia hufanya kazi kwa karibu na Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Jaji Mkuu na taasisi nyingine za kisheria ili kuhakikisha mfumo wa Mahakama unakuwa na rasilimali watu wenye weledi na maadili. Kwa ujumla, Tume ya Utumishi wa Mahakama ni mhimili muhimu katika kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati na kwa usawa.

MAMBO ya Muhimu Fomu ya Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama June 2025

Baada ya kujisajiri na kuingia kwenye mfumo wa ajira tume ya utumishi wa Mahakama utaletewa fomu ya kujaza ya kutuma maombi ya kazi baada ya kuchagua kazi unayotaka kutuma maombi yako.

Hapa chini ni vitu vyote vya msingi vilivyopo kwenye fomu ya maombi ya kazi tume ya utumishi wa mahakama

A) Taarifa Binafsi(Persoal Details)

  • Majina matatu
  • Tarehe ya kuzaliwa
  • Jinsia na hali ya ndoa
  • Mahari unapoishi,Mkoa na namba ya simu
  • Kitambusho cha Taifa,Pasport Size na cheti cha kuzaliwa

B) Taarifa za Kitaaluma

  • Taarifa za kidato cha nne
  • Taarifa za kidato cha sita
  • Taarifa za elimu ya juu

C) Taarifa za kuajiriwa

  • Kama umeajiwa au hujaajiriwa

Hizo ndio taarifa zote utakazoobwa katika fomu ya maombi ya ajira kwenye mfumo wa Ajira Tume ya Utumishi wa Mahakama.

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!