NAFASI za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro June 2025

Kwa AJIRA Mpya Kila Siku (BOFYA HAPA)

_____________________________________

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya Mwaka 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 na kibali cha Ajira Mbadala
chenye Kumb.Na. FA.228/613/01G/049 cha tarehe 14/04/2025. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-

NAFASI za Kazi Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro June 2025

DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 11

KAZI NA MAJUKUMU

i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari,
iv. Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote,
v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
vi. Kufanya usafi wa Gari,
vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha
magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Halmashauri ya Manispaa Morogoro, S.L.P 166, 2 Station Road, 67182, Morogoro, Simu/Nukushi Na: +255 023 2935242,Tovuti: www.morogoro.go.tz, Barua Pepe: [email protected]

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 4

KAZI NA MAJUKUMU

i. Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming correspondence register)
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register)
iii. Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers)
iv. Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji
v. Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa
vi. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)

SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Utunzaji wa kumbukumbu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C

MASHARTI YA JUMLA

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
iii. Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Diploma/Certificates, – Cheti cha Halmashauri ya Manispaa Morogoro, S.L.P 166, 2 Station Road, 67182, Morogoro, Simu/Nukushi Na: +255 023 2935242,Tovuti: www.morogoro.go.tz, Barua Pepe: [email protected] mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma.
iv. “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 11 Juni, 2025.

Leave your thoughts

Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Tanzania (St John’s University of Tanzania – SJUT) ni chuo kikuu binafsi kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Tanzania. Kimeanzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya juu yenye msingi wa maadili, maono na huduma kwa jamii. Kiko katika mji wa Dodoma, katikati ya Tanzania, na kinatoa programu mbalimbali kuanzia shahada za kwanza hadi za juu
Smiles Dental Clinic ni kliniki ya kisasa ya meno inayotoa huduma bora kwa wagonjwa wa rika zote. Kliniki hii imejipatia sifa kwa kutumia vifaa vya kisasa na teknolojia ya hali ya juu katika kutibu matatizo mbalimbali ya meno kama vile kung’oa, kusafisha, kuweka dawa, na kufunga braces. Madaktari wake ni wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika fani ya afya ya kinywa
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 25-05-2025 na tarehe 05-06-2025 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi
Angalia Majina ya Walioitwa Kazini Kupitia UTUMISHI – Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) 2025 Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) ni chombo cha serikali chenye hadhi ya Idara Huru kilichoanzishwa mahsusi kurahisisha mchakato wa ajira kwa watumishi wa umma. Sekretarieti hii ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002
error: Content is protected !!