Close Menu
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Kisiwa24Kisiwa24
  • Home
  • Ajira
  • Michezo
  • Makala
Subscribe
Kisiwa24Kisiwa24
Home»Ajira»Nafasi 8 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngara May 2025
Ajira

Nafasi 8 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngara May 2025

Kisiwa24By Kisiwa24May 30, 2025No Comments4 Mins Read
Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara amepokea kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilichotoa idhini ya utekelezaji wa nafasi za Ajira Mpya katika ikama ya mwaka wa fedha 2024/2025 chenye Kumb. Na. FA. 97/228/01/A/25 cha tarehe 29 Aprili, 2025. Hivyo anapenda kuwatangazia watanzania wote wenye sifa kutuma maombi ya kazi katika nafasi zifuatazo:-

Nafasi 8 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Ngara May 2025

MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 4

KAZI NA MAJUMKUMU

i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri,
ii.Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa;
iii. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi;
iv. Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Divisheni, Vitengo na Sehemu zinazohusika;
v.Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
vi. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali; na
vii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

SIFA ZA MUOMBAJI

Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) na amehitimu Stashahada/Diploma ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa Dakika Moja na kupata program za kompyuta za ofisi kama vile:- Word, Excel, Power Point, Internet, Email, na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C 1

MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 04

KAZI NA MAJUMKUMU

i. Kuorodhesha barua zinazoingia masijala kwenye Rejista (Incoming Correspondence Register)
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (Outgoing Correspondence Register).
iii. Kusambaza majalada kwa Watendaji (Action Officers).
iv. Kupokea Majalada kutoka kwa Watendaji (Action Officers).
v. Kupokea majalada yanayorudi kutoka kwa Watendaji.
vi. Kurudisha masijala kwenye Shabaka/ Kabati la Masijala (Racks/Filling Cabinets) au mahala pengine yanapohifadhiwa.
vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (File Tracking).

SIFA ZA MUOMBAJI

Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI). Awe na cheti cha Stashahada (Diploma) (NTA LEVEL 6) cha utunzaji wa kumbukumbu katika fani ya Utunzaji wa Kumbukumbu
kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, na mwenye ujuzi wa Kompyuta.

NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS C 1

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

i. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 na umri usiopungua miaka 18,
ii. Waombaji waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa,
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye Anuani, Namba za Simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees) wa kuaminika,
iv. Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya Kidato cha Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye Ajira Portal, Testimonials “Provision Results”, “Statement of Results” Hati ya Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita HAVIKUBALIKI,
v. Waombaji wote waweke picha mbili “Passport Size” ya hivi karibuni katika ukurasa wa Ajira Portal,
vi. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika yaani TCU, NECTA na NACTE,
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi,
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katikan Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka wenye Kumb. Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010,
ix. Uwasilishwaji taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria,
x. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Juni, 2025, MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu na anuani.

  • BONYEZA HAPA KUPAKUA TANGAZO LOTE

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
Previous ArticleNafasi 15 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Biharamulo May 2025
Next Article Majina ya Walioitwa Kazini Halmashauri Ya Manispaa Ya Kinondoni Na Temeke 30 Mei 2025
Kisiwa24

Related Posts

Ajira

MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM

December 13, 2025
Ajira

NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited

December 13, 2025
Ajira

NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania

December 13, 2025
Add A Comment
Leave A Reply Cancel Reply

Recent Posts

  • MAJINA Walioitwa Kazini Chuo Kikuu Cha UDSM
  • NAFASI za Kazi Equity Bank Tanzania Limited
  • NAFASI Za Kazi DTB Bank Tanzania
  • NAFASI za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
  • NAFASI za Kazi Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania

Recent Comments

No comments to show.
Demo
Top Posts

Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2025

July 12, 20251,178 Views

MAJINA Walioitwa Kwenye Usaili MDAs & LGAs

December 6, 2025788 Views

NAFASI za Kazi Za Mkataba Wizara Ya Maliasili Na Utalii

December 6, 2025446 Views
Stay In Touch
  • Facebook
  • YouTube
  • TikTok
  • WhatsApp
  • Twitter
  • Instagram
Latest Reviews

Subscribe to Updates

Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

Demo
© 2025 Kiswa24 Blog. Designed by Kisiwa24.

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.