Tetesi za Usajili Simba Sc 2024/2025
Hapa chini ni baadhi ya wachezaji wanaohusishwa moja kwa moja kuweza kusajiliwa na klabu ya Simba kwa msimu huu mpya wa 2024/2025 kwenye dirisha kubwa la usajili
1. Debora Fernandes Mavumbo
Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba kwa sasa iko katika hatua za ukingoni kabiasa kukamilisha na kuinasa saini ya mchezaji Debora Fernandes Mavumbo amabye anacheza nafasi ya kiungo akitokea klabu ya Mutondo Stars ya nchini Zambia kwa mkataba wa miaka miwili.
2. Nathan Fasika Idumba
Nje ya Debora Fernades pia Simba Sc klabu iko mbioni kumsajili mlinzi wa kimataifa wa nchini DR Congo Nrthan Fasika Idumba. Inasemekana klabu ya Simba tayari imesha fanya mazungumuzo na wawakilishi wa mlinzi huyo ili kuweza kuitumikia klabu hiyo.Idumba mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa anaitumikia klabu ya Valerenga ya nchini Norway kwa mkopo akitokea klabu ya Cape Town City ya nchini Afrika Kusini.
3. Aubin Kramo Kouamé
Kwa winga Aubin Kramo Kouamé yeye tayari amesha ongea na klabu ya Simba na kua bado ataendelea kuwa mali ya wekundu wa msimbazi. Kouamé mwenye umri wa miaka 25 ambaye kwa sasa ni majeruhi pindi atakapopona na kurudi uwanjani ataendelea kuitumikia klabu hiyo
4. D’Avila Messi Kessie Simba SC
Simba pia iko katika mikakati ya kuhakikisha inaimarisha kikosi chake kwa msimu huu huku ikiwa mbioni kumsajri D’Avila Messi Kessie ambaye ni winga kutokea nchini Ivory Coast katiaka klabu ya Inova Sporting Club Association. D’Avila ni miongoni mwa winga wakali kwani msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao takribani 11 na kutoa pasi za mabao 6 akiwa na klabu yake.
5. Ayoub Lakred
Kutokana na huduma yake nzuri kwa msimu uliopita katiak klabu ya Simba, Klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi imepanga kumwongezea mkataba wa mwaka 1 golikipa wake Ayoub Lakred hadi mwaka 2025. Lakred mwenye umri wa miaka 28 akiwa raia wa Morocco kwa msimu huu wa 2024/2025 ataendelea kuitumikia klabu ya Simba.
6. Augustine Okejepha
Simba imeingia kwenye kinyang’anyiro cha kuisaka saini ya kiungo wa ulinzi wa klabu ya Rivers Utd Augustine Okajepha kwa kuweka dau la USD 200,000 japo kua ofa hiyo imeonekana kuwa ndo na klabu hiyo imehitaji USD 270,000 ili tu kuweza kumwachia mchezaji huyo kujiunga na klabu ya Simba
7. Rahim Shomary
Simba imepiga hodi kwa klabu ya KMC FC kwa maongezi ya kutaka kunasa beki wa kushoto Rahimu Shomary mwenye umri wa miaka 19 ikiwa ni mipango ya kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya timu hiyo kuelekea msimu mpya wa 2024/2025.
8. Damaro Camara
Bado Simba inazidi kuvuka mipaka hadi kuingia Hafia ya Guinea lengo ni kuanzisha mazungumzo ya kuweza kuipa huduma ya mchezaji Damora Camara kiungo mkabaji ambaye wakati mwingine anawez kutumika kama beki wa kati
9. Joshua Mutale
Simba imetia nia na kwa sasa imefikia katika hatua za mwisho kabisa katika kumsajili winga kututokea Power Dynamos ya nchini Zambia Joshua Mutale mwenye umri wa miaka 22
10. Valentin Nouma
Mikakati ya klabu ya Simba katiak kuimalisha kikosi cha ke kwenye msimu huu mpya umeifanya klabu hiyo kwenda hadi FC Saint Eloi Lupopo ya DR Congo kwa lengo la kufanya mazungumzo na klabu hiyo ili kumsajili beki wa kushoto wa klabu hiyo raia wa Burkina Faso Valentin Nouma mwenye umri wa miaka 24.
11. Joyce Lomalisa
Simba wamegonga hodi kwa watani wao wa jadi Yanga na kuanza kufanya mazungumzo ya kuhitaji saini ya beki Joyce Lomalisa aliyemaliza mkataba wake ndani ya Yanga.

Mapendekezo Ya Mhariri
>>Ligi Bora Africa 2024 | Viwango vya ubora CAF Ranking
>>Ratiba ya treni za SGR Dar es Salaam na Morogoro