Nafasi za Kazi Hospitali ya Taifa ya Mirembe

Filed in Ajira by on March 22, 2026 0 Comments

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe anawatangazia uwepo wa nafasi za kazi kwa Ajira ya Mkataba wa Kujitolea.

Nafasi hizo zinahusu kada zifuatazo;

  • Maafisa Wauguzi Wasaidizi (ANO), nafasi kumi na nne (14).
  • Wasaidizi wa Afya (MATT) nafasi kumi (10).
  • Dereva, nafasi moja (1) na Afisa Habari nafasi moja (1).

Watanzania wenye sifa ya kuomba, na kujaza nafasi hizi, wanaombwa kuleta maombi ya:

✅AFISA MUUGUZI MSAIDIZI
Mwombaji awe na stashahada ya Uuuguzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, vyeti vya Uuguzi na Ukunga na leseni hai.

✅MSAIDIZI WA AFYA
Mwombaji awe na cheti kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali,

✅DEREVA
Mwombaji awe na cheti kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na leseni hai.

✅AFISA HABARI
Mwombaji awe na stashahada au shahada kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali

SIFA ZA JUMLA

  • Awe na umri usiozidi miaka 35 (Thelathini na tano).
  • Awe amefaulu kidato cha Nne / Sita.
  • Awe na kitambulisho cha Uraia na
  • Awe na wadhamini wawili wanaotambulika na Serikali ya Kijiji/ Mtaa anapoishi.

MASHARTI YA JUMLA
Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kidato cha Nne / Sita, cheti cha taaluma, cheti cha kuzaliwa, maelezo binafsi (curriculum Vitae).

Waombaji watakaowasilisha “Result Slip”, “Statement of Result”, “Provisional Result” au “Transcript” HAWATAKUBALIWA.

Maombi yote yatumwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe,
S.L.P 910.
DODOMA
Au kupitia barua pepe: barua@mirembe.or.tz

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 08 Aprili, 2026, Saa 9:30 Alasiri.

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *