Close Menu
Kisiwa24

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    What's Hot

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026
    Kisiwa24Kisiwa24
    • Home
    • Ajira
    • Michezo
    • Makala
    • Elimu
    Kisiwa24
    Home»Ajira»NAFASI Za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Handeni June 2025
    Ajira

    NAFASI Za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Handeni June 2025

    Kisiwa24By Kisiwa24June 4, 2025No Comments4 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

    NAFASI Za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Handeni June 2025

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
    Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-

    MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 4

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata program za compyuta za ofisi kama vile: – Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

    KAZI NA MAJUKUMU

    i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri;
    ii. Kupokea wageni na kuwasiliza shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
    iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
    iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi; Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, S.L.P 355, Handeni, Simu: +255 0272977402, Nukushi: +255 0272977402, Barua pepe: ded@handenidc.go.tz, Tovuti: www.handenidc.go.tz
    v. Kupokea majalada na kusambaza kwa maafisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
    vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinahusika;
    vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
    viii.Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

    NGAZI YA MSHAHARA

    Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

    DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 7

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), mwenye leseni Daraja “E” au “C” ya uendeshaji Pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali

    MAJUKUMU YA KAZI

    i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
    ii. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
    iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
    iv. Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote;
    v. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
    vi. Kufanya usafi wa Gari na
    vii. Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake

    NGAZI YA MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS B.

    MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

    i. Waomabji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale walioko kazini Serikalini
    ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye Mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
    taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, S.L.P 355, Handeni, Simu: +255 0272977402, Nukushi: +255 0272977402, Barua pepe: ded@handenidc.go.tz, Tovuti: www.handenidc.go.tz
    iii. Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Details Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
    iv. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia Sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya kazi
    kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
    v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detail C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika Pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
    vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika;
    vii. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, Computer Certificates, Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate
    from Respective Boards);
    viii. Testimonial, “Provisional Results”, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
    ix. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
    x. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi
    xi. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
    xii. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
    xiii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 16/06/2025

    • BONYEZA HAPA KUTUMA MAOMBI

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleNAFASI Za Kazi Lake Victoria Fisheries Organization June 2025
    Next Article PDF: MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Halmashauri Mbalimbali Leo UTUMISHI
    Kisiwa24

    Related Posts

    Ajira

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026
    Ajira

    NAFASI 33 za Kazi Chuo Cha MUST

    January 3, 2026
    Ajira

    NAFASI 10 za Kazi Halmshauri ya Mji Babati

    January 3, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    Demo
    Top Posts

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202560 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202537 Views

    Jinsi ya kuangalia Namba ya leseni ya udereva

    March 9, 202537 Views
    Stay In Touch
    • Facebook
    • YouTube
    • TikTok
    • WhatsApp
    • Twitter
    • Instagram
    Latest Reviews

    Subscribe to Updates

    Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

    Demo
    Most Popular

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202560 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202537 Views

    Jinsi ya kuangalia Namba ya leseni ya udereva

    March 9, 202537 Views
    Our Picks

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    • Home
    • Buy Now
    © 2026 ThemeSphere. Designed by ThemeSphere.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.