Close Menu
Kisiwa24

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    What's Hot

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026
    Kisiwa24Kisiwa24
    • Home
    • Ajira
    • Michezo
    • Makala
    • Elimu
    Kisiwa24
    Home»Ajira»Nafasi 9 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Chalinze June 2025
    Ajira

    Nafasi 9 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Chalinze June 2025

    Kisiwa24By Kisiwa24June 2, 2025No Comments4 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa ya kujaza nafasi zilizotolewa na kibali chenye Kumb.Na FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

    Nafasi 9 za Kazi Halmashauri Ya Wilaya Ya Chalinze June 2025

    MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II (Office Management Secretary II) – NAFASI 05

    KAZI NA MAJUKUMU

    i. Kuchapa barua, taarifa, nyaraka za kawaida na za siri.
    ii. Kupokea wageni na kuwasaidia shida zao na kuwaelekeza wanapoweza kusaidiwa.
    iii. Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
    iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
    v. Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
    vi. Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
    vii. Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
    viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi na
    ix. Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Stashahada/Diploma (NTA Level 6) ya Uhazili na awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata Progamu ya Kompyuta za Ofisi kama vile Word, Excel, Powerpoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

    NGAZI YA MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali ya TGS C kwa mwezi

    DEREVA DARAJA LA II (Driver II) -NAFASI 04

    KAZI NA MAJUKUMU

    i. Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za udereva.
    ii. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali kwa kuzingatia maelekezo utakayopewa na msimamizi wako wa kazi.
    iii. Kutunza na kuandika daftari la safari (log-book) kwa safari zote.
    iv. Kufanya matengenezo ya madogo madogo ya magari
    v. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na
    vi. Kutekeleza kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

    SIFA ZA MWOMBAJI

    Awe na elimu ya Kidato cha nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) awe na lesseni
    Daraja C au E ya uendeshaji wa magari, ambayo ameifanyia kazi kwa muda
    usiopungua mwaka mmoja, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na VETA au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

    NGAZI YA MSHAHARA

    Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali ya TGS B kwa mwezi.

    MASHARTI KWA JUMLA

    i. Mwombaji awe Raia wa Tanzania ambaye ana umri si zaidi ya miaka 45 na sio pungufu ya Miaka 18.
    ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
    iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum
    Vitae (CV) yenye Anwani inayotumika, namba ya simu na Anuani ya barua pepe (E- mail address) pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
    iv. “Provisional/Testimonials/Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha nne na sita (form IV na VI result slip) HAVITAKUBALIWA.
    v. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
    vi. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokua kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
    vii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na Wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
    viii. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbali mbali
    kwa kuzingatia sifa za kazi husika, Postgraduate/degree/advanced diploma/diploma/Certificates, Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI,
    Compture certificate, Vyeti vya taaluma. (Proffessional Certificate from respective Board)
    ix. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA)
    x. Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
    xi. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza
    xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15/06/2025
    xiii. MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

    • BONYEZA HAPA KUPAKUA TANGAZO KAMILI

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMATOKEO ya Usaili Wa Vitendo Uliofanyika Tarehe 01 June 2025
    Next Article NAFASI za Kazi Airtel Tanzania June 2025
    Kisiwa24

    Related Posts

    Ajira

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026
    Ajira

    NAFASI 33 za Kazi Chuo Cha MUST

    January 3, 2026
    Ajira

    NAFASI 10 za Kazi Halmshauri ya Mji Babati

    January 3, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    Demo
    Top Posts

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202554 Views

    Jinsi Ya Kupata Prem Number Kwa Urahisi Tanzania

    July 15, 202531 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202530 Views
    Stay In Touch
    • Facebook
    • YouTube
    • TikTok
    • WhatsApp
    • Twitter
    • Instagram
    Latest Reviews

    Subscribe to Updates

    Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

    Demo
    Most Popular

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202554 Views

    Jinsi Ya Kupata Prem Number Kwa Urahisi Tanzania

    July 15, 202531 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202530 Views
    Our Picks

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    • Home
    • Buy Now
    © 2026 ThemeSphere. Designed by ThemeSphere.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.