Close Menu
Kisiwa24

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    What's Hot

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026
    Kisiwa24Kisiwa24
    • Home
    • Ajira
    • Michezo
    • Makala
    • Elimu
    Kisiwa24
    Home»Makala»Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
    Makala

    Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa

    Kisiwa24By Kisiwa24November 5, 2024No Comments5 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

    Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa,  Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imekua ikitangaza nafasi za kazi ya mtendaji wa kijiji na mitaa kwa wilaya mbalimbali nchini Tanzania. Kama wewe ni miongoni mwa waliokidhi vigezo vya kua mtendaji wa mtaa au kijiji basi huna budi kuweza kujua muundo wa barua ya kuomba kazi ya mtendaji wa kijiji au mtaa inavyoandikwa.

    Nafasi nyingi za kazi za Mtendaji wa kijiji katika halmashauri za wilaya mbalimbali nchini Tanzania mara nyingi huitaji mwombaji aliyeweza kuhitimu angalau elimu ya kidato cha nne (form iv) au kidato cha sita (form six) aliyehitimu astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo:

    • Utawala
    • sheria
    • Elimu ya jamii
    • usimamizi wa fedha
    • maendeleo ya jamii na sayansi ya sanaa

    kutoka chuo cha serikali za mitaa hombolo au chuo chochote kinachotambuliwa na serikali.

    Kama wewe ni miongoni mwa wenye sifa hizo hapo juu basi unaweza kutuma maombi pindi ajira hizo za mtendaji wa kijiji na mitaa zinapotangwazwa kupitia Halmashauri husika au kwa kutumia tovuti ya Ajira Portal. Lakini kabla hujatuma maombi yako basi ni muhimu kufahamu zaidi juu ya muundo wa uandishi wa barua ya maombi ya kazi kwa kada hiyi ya mtendaji wa kijiji na Mtaa.

    Kwa kuliona hilo na kujali mahitaji ya wafuasi wetu basi ndio maana sisi Habarika24 tumeamua kukuonyesha mfano/muundo wa barua ya kuamba kazi ya mtendaji wa kijiji na mtaa.

    Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji
    Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji

    Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa

    Barua ya kuomba kazi ndio waraka ambao mara nyingi husomwa kabla ya waraka mwingine wowote unaoambatanishwa katika kuomba kazi. Ni vyema barua hii ikaandaliwa kwa umakini, na kwa kufuata alama za kiuandishi huku ikijaribu kugusa kwa ufupi mambo yaliyoonekana kwenye wasifu binafsi.

    Kuandika barua ya maombi ya kazi ni hatua muhimu sana katika mchakato wa kuomba kazi ya mtendaji wa kijiji na mtaa. Barua yako inapaswa kuwa ya kipekee, rasmi, na yenye maelezo ya kina kuhusu sifa na uzoefu wako.

    Hatua za Uandishi wa Barua

    Hapa chini ni muundo wa barua rasmi ya kuomba kazi katika ngazi ya Mtendaji wa Kijiji na Mtaa

    1. Taarifa za Muombaji ( Anuani ya Mwandishi)

    Anza barua yako kwa kuandika jina lako kamili, anuani, namba ya simu, na barua pepe. Hii itafuatiwa na tarehe ambayo unaandika barua hiyo.

    2.  Taarifa za Mpokeaji (Anuani ya Mwandikiwa)

    Hapa hukaliwa na anuani ya mwandishi.Andika jina kamili la anayepokea barua, cheo chake, na anuani ya ofisi husika.

    3. Utangulizi

    Katika aya ya kwanza, taja nafasi unayoomba na jinsi ulivyogundua nafasi hiyo. Eleza kwa kifupi kwanini unafikiri wewe ni mgombea bora.

    4. Sifa na Uzoefu

    Toa maelezo ya kina kuhusu elimu yako, uzoefu wa kazi, na sifa nyinginezo zinazokufanya uwe mgombea bora kwa nafasi hiyo. Eleza jinsi sifa zako zinavyolingana na mahitaji ya nafasi unayoomba.

    5. Hitimisho

    Hitimisha barua yako kwa kueleza shukrani kwa kuzingatia ombi lako na taja kwamba uko tayari kwa mahojiano wakati wowote utakaohitajika. Weka sahihi na jina lako

    Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Mtendaji wa Kijiji na Mtaa

     

    Juma Saidi Kibwagizo

    Simu; 07872377141

    Dar es Salaam, Tanzania

    12/06/2005

     

    Mtendaji Mkuu wa Wilaya,

    Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha,

    S.L.P  30153,

    Kibaha.

    YAH: MAOMBI YA KAZI YA MTENDAJI WA KIJIJI/MTAA

    Ndugu,

    Nachukua fursa hii kuomba nafasi ya kazi ya Mtendaji wa Kijiji/Mtaa iliyotangazwa kupitia tangazo lenu la tarehe 10/06/2005 kupitia tovuti ya Ajira portal.

    Nina shahada ya elimu kutoka chuo kikuu cha Dodoma niliyohitimu mwaka 2000. Nina uzoefu wa miaka 3 katika masuala ya utawala na uongozi wa jamii. Nimewahi kufanya kazi kama afisa rasilimali watu.

    Ninaamini nina sifa zote zinazohitajika kwa nafasi hii, ikiwa ni pamoja na:
    – Uwezo wa kuongoza na kusimamia shughuli za maendeleo ya jamii
    – Ujuzi wa kutumia kompyuta na teknolojia ya habari
    – Uwezo wa kufanya kazi chini ya masharti magumu
    – Uwezo wa kufanya kazi bila usimamizi wa karibu
    – Uzoefu katika usimamizi wa fedha na rasilimali

    Ninaahidi kutumia ujuzi na uzoefu wangu kusaidia maendeleo ya jamii na kutoa huduma bora kwa wananchi.

    Nimeambatanisha nyaraka zifuatazo:
    1. Wasifu (CV)
    2. Nakala za vyeti vya elimu
    3. Nakala za vyeti vya mafunzo
    4. Barua za mapendekezo
    5. Picha ya hivi karibuni

    Nasubiri majibu yenu.

    Wako mtiifu,

    …………………….
    Juma Saidi Kibwagizo
    Simu: 07872377141
    Barua pepe: kibwagizo@gmail.com

    Mapendekezo ya Mhariri;

    1. Ratiba ya treni za SGR Dar es Salaam na Morogoro

    2. Soma Nauli za treni ya mwendokasi SGR

    3. JINSI ya Kutumia Kadi Ya GUSA AzamPesa

    4. Jinsi Ya Kufanya Biashara Mtandaoni

    5. Jinsi Ya Kuhakiki Bima Ya Gari Lako Haraka Zaidi

    Asante kwa kusoma makala yetu hadi mwisho, ikiwa unamaswali yoyote tafadhali acha maoni hapa chini au unaweza Wasiliana nasi. Usisahau kujiunga nasi kwenye WhatsApp gropu letu kwa updates zaidi.

    Jiunge na Whatsap Gropu letu kwa updates za kila siku

    BONYEZA HAPA

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleRatiba ya Mashindano ya Ngao ya Jamii 2024/2025
    Next Article Jezi Mpya Ya Yanga Sc Msimu Wa 2024/2025
    Kisiwa24

    Related Posts

    Makala

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026
    Makala

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 2025
    Makala

    Jinsi ya kupika Pilau kwenye Rice Cooker

    October 9, 2025
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    Demo
    Top Posts

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202558 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202532 Views

    Jinsi Ya Kupata Prem Number Kwa Urahisi Tanzania

    July 15, 202532 Views
    Stay In Touch
    • Facebook
    • YouTube
    • TikTok
    • WhatsApp
    • Twitter
    • Instagram
    Latest Reviews

    Subscribe to Updates

    Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

    Demo
    Most Popular

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202558 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202532 Views

    Jinsi Ya Kupata Prem Number Kwa Urahisi Tanzania

    July 15, 202532 Views
    Our Picks

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    • Home
    • Buy Now
    © 2026 ThemeSphere. Designed by ThemeSphere.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.