Close Menu
Kisiwa24

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    What's Hot

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026
    Kisiwa24Kisiwa24
    • Home
    • Ajira
    • Michezo
    • Makala
    • Elimu
    Kisiwa24
    Home»Ajira»Nafasi Mpya 15 Za Kazi Halimashauri Ya Manispaa Ya Tabora
    Ajira

    Nafasi Mpya 15 Za Kazi Halimashauri Ya Manispaa Ya Tabora

    Kisiwa24By Kisiwa24August 30, 2024No Comments6 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Reddit Telegram Email
    Share
    Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

    Nafasi Mpya 15 Za Kazi Halimashauri Ya Manispaa Ya Tabora

    Tangazo

    Habari hii na nyingine nyingi zinapatikana kwenye telegram channel yetu na WhatsApp channel yetu tumia linki hapo chini kujiunga

    BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA TELEGRAM CHANNEL YETU

    BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA WHATSAPP CHANNEL YETU

    Mkurugenzi wa Manispaa amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-

    Nafasi Mpya 15 Za Kazi Halimashauri Ya Manispaa Ya Tabora

    Nafasi Mpya 15 Za Kazi Halimashauri Ya Manispaa Ya Tabora

    DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 05)

    KAZI NA MAJUKUMU
    i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
    ii. Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi
    iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari
    iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
    v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari ( log book)
    vi. Kufanya usafi wa gari

    SIFA ZA KUAJIRIWA
    Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe naleseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari
    (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

    NGAZI YA MSHAHARA
    Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B

    MTENDAJI WA MTAA lll – NAFASI (05)

    MAJUKUMU YA KAZI
    i. Kuwa Afisa Masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Mtaa
    ii. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao,Kuwa Mlinzi wa amani
    na msimamizi wa utawala bora katika Mtaa
    iii. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji mipango ya maendeleo ya Mtaa
    iv. Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Mtaa
    v. Kutafsiri na kusimamia Sera,sheria na Taratibu
    vi. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoanjaa,umasikini na kuongeza uzalishaji mali.
    vii. Kiongozo wa wakuu wa vitengo vya kitaaluma katika jamii
    viii. Kusimamia,kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Mtaa
    ix. Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Mtaa.
    x. Kusimamia utungaji wa sheria ndogondogo za Mtaa
    xi. Kupokea,kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
    xii. Kusimamia ukusanyaji wa mapato ndani ya Mtaa na kusoma mapato na matumizi kila baada ya miezi miwili ambapo kwa mwaka utakuwa na mikutano sita (6)
    xiii. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata

    SIFA ZA KUAJIRIWA

    Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha nne/sita na aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

    NGAZI YA MSHAHARA
    Kwa kuzingatia ngazi za Mshahara ya Serikali – TGS B

    MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI TANO (05)

    MAJUKUMU YA KAZI

    i. Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji;
    ii. Katibu wa Kamati ya kijiji;
    iii. Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Kijiji;
    iv. Mshauri wa Kamati ya Kijiji kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Kijiji;
    v. Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Kijiji;
    vi. Msimamizi wa Mtekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umasikini katika Kijiji;
    vii. Msimamizi wa Mtekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umasikini katika Kijiji;
    viii. Kusimamia Ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi; na
    ix. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

    SIFA ZA KUAJIRIWA
    Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI), awe amehitimu mafunzo ya Astashahada katika moja ya fani zifuatazo; Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

    MSHAHARA
    Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS B.

    MASHARTI YA JUMLA

    i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini – Serikalini.
    ii. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira aina ya Ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
    iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza Curriculum Vitae (CV) yenye Anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya barua pepe (E-mail adress) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
    “Provisional “/Testimonials”/ “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha Nne na Sita (Form IV and Form VI results slip)

    HAVITAKUBALIWA.
    iv. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
    v. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
    vi. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wao wajiridhishe ipasavyo.
    vii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma, wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
    viii. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    ix. Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Dilpoma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma (Professional Certificate from Respective Boards).
    x. Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA au NACTVET).
    xi. Uwasilishaji wa Taarifa na Sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
    xii. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.
    xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Septemba, 2024.
    xiv. MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:

    Mkurugenzi wa Manispaa, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora,
    Mtaa wa Ikulu,4Barabara ya Kiwanja cha Ndege,
    S.L.P 174,45182 TABORA.

    xv. Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (RecruitmentPortal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa “Recruitment Portal”
    xvi. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKILIWA.

    Mapendekezo Ya Mhariri;

    1. Tangazo La Kuitwa Kwenye Usahili Kada Ya Afya Septemba 2024

    2. Nafasi Mpya 15 Za Kazi Kutoka Halmashauri ya Manispaa Ya Tabora

    3. Nafasi Mpya 15 Za Kazi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino

    4. Nafasi Mbali Mbali Za kazi zilizotangazwa Agosti

    5. Nafasi Mpya Za Kzi Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala

    6. Nafasi Mpya 27 Za Kazi Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleTangazo La Kuitwa Kwenye Usahili Kada Ya Afya Septemba 2024
    Next Article Nafasi Mpya 32 za Kazi Kutoka Taasisi Ya Utafiti Wa Misitu Tanzania Septemba 2024
    Kisiwa24

    Related Posts

    Ajira

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026
    Ajira

    NAFASI 33 za Kazi Chuo Cha MUST

    January 3, 2026
    Ajira

    NAFASI 10 za Kazi Halmshauri ya Mji Babati

    January 3, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    Demo
    Top Posts

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202560 Views

    Jinsi ya kuangalia Namba ya leseni ya udereva

    March 9, 202537 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202535 Views
    Stay In Touch
    • Facebook
    • YouTube
    • TikTok
    • WhatsApp
    • Twitter
    • Instagram
    Latest Reviews

    Subscribe to Updates

    Get the latest tech news from FooBar about tech, design and biz.

    Demo
    Most Popular

    Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi ya Sheli

    July 2, 202560 Views

    Jinsi ya kuangalia Namba ya leseni ya udereva

    March 9, 202537 Views

    Link Za Magroup Ya WhatsApp Tanzania 2026

    December 21, 202535 Views
    Our Picks

    Fomu za Kujiunga Kidato cha Kwanza 2026 – TAMISEMI Form One Joining Instructions

    January 4, 2026

    RATIBA Mpya ya Treni Za SGR Dar, Morogoro hadi Dodoma 2026

    January 4, 2026

    NAFASI 07 za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

    January 3, 2026

    Subscribe to Updates

    Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    • Home
    • Buy Now
    © 2026 ThemeSphere. Designed by ThemeSphere.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.